Na
Mwandishi wa Idara ya habari maelezo
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete ametunukiwa tuzo na Taasisi ya Kimataifa ya Gavi
Alliance kutokana na mchango wake mkubwa kwa jamii wa kuhakikisha kuwa vifo vya
kina mama wajawazito na watoto vinavyotokana na tatizo la uzazi vinapungua hapa
nchini.
Tuzo hiyo
ilitolewa jana usiku katika Hoteli ya Serena na Mwenyekiti wa bodi ya Taasisi
hiyo Dagfinn Hoybraten wakati wa hafla ya utoaji tuzo ilienda sambamba na
mkutano wa kimataifa wa siku tatu wa Gavi Alliance unaoendelea jijini Dar es
Salaam.
Akiongea
kabla ya kukabidhiwa tuzo hiyo Mwanamuzi maarufu wa Afrika ya Kusini
Yvonne Chakachaka ambaye pia ni Balozi wa heshima wa Shirika la Umoja wa
Mataifa la Kushughulikia watoto Duniani (UNICEF) na mshereheshaji wa shughuli hiyo
alisema kuwa hivi sasa wake wa marais wamekuwa wakijitoa kuisaidia jamii hasa
katika mambo yahusuyo afya ya mama wajawazito na mtoto.
Mke wa
rais wa Zambia Dk. Christine Kaseba Sata naye alipewa tuzo kama aliyopewa
Mama Kikwete.
Aidha
Wizara za Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na Fedha zilipewa tuzo kwa ajili ya
kuandaa mkutano huo wa kimataifa wa Umoja wa wadau wa chanjo na Kinga Duniani
uliohudhuriwa na wataalamu wa afya, mawaziri wa afya na wake wa marais
kutoka barani Afrika.

0 comments:
Post a Comment